Sakata la watumishi wa umma kushughi vyeti vya elimu limezidi kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000.
Hatua
hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao, 1,951
wana vyeti vya kughushi.
Kuongezeka
kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli, wiki
iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali ambao
wamebainika kuwa na vyeti feki.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki ni zaidi ya 9,000 na anaisubiri ripoti hiyo kuifanyia kazi.
“Kwa
hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi
hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali
unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu
mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisema Rais Magufuli.
Akiwasilisha
hotuba ya bajeti ya mwaka 2017/18 kwa ofisi yake jana bungeni mjini
hapa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema baada ya kubainika kwa hali hiyo,
wahusika waliondolewa kwenye mchakato, huku vyeti hivyo vikiwasilishwa
katika mamlaka husika kwa hatua za kisheria.
“Wahusika
waliondolewa katika mchakato pamoja na vyeti hivyo kuchukuliwa na
kuwasilishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Kairuki.
Hata
hivyo, zipo taarifa zinazodai kuwa orodha ya watumishi wa umma ambao
wamebainika kuwa na vyeti feki itawekwa hadharani Aprili 30.
Zaidi
inaelezwa kuwa sakata hilo la vyeti feki linawagusa pia mabalozi ambao
ni wawakilishi wa Watanzania katika mataifa mbalimbali, wakuu wa wilaya
na mikoa.
JAMII VIEWER
0 comments:
Post a Comment