Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limemruhusu beki mpya wa pembeni, Hassan Kessy na wachezaji wenzake wapya, Vicent Andrew ‘Dante’, Juma Mahadhi na Beno Kakolanya kuwavaa MO Bejaia.
Yanga iliwaongeza wachezaji hao hivi karibuni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kinachoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika. Kessy aliyetokea Simba amekuwa ni kati ya mabeki bora zaidi kwenye soka hapa Tanzania.
Timu hiyo, iliyopo kambini nchini Uturuki itaavana na MO Bejaia keshokutwa Jumapili katika Uwanja wa Unite Maghrebin mjini Bejaia, Algeria.
Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema juzi jioni walipokea leseni za wachezaji hao kutoka Caf za kuwaruhusu kucheza mechi hiyo hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu.
“Jana (Jumatano) jioni tulipokea barua Caf ikiwaruhusu wachezaji wanne waliosajiliwa na Yanga ambao majina yao yalitumwa Caf kucheza mechi dhidi ya MO Bejaia.
“TFF tayari imeitaarifu Yanga kwa njia ya barua kuwa ni ruksa kuwatumia wachezaji hao kama wakihitaji baada ya kupokea baraka kutoka Caf.
“Majina ya wachezaji hao tuliyatuma hivi karibuni kabla usajili huo haujafunguliwa na yalipitishwa na Caf baada ya usajili huo kufunguliwa,” alisema Lucas.
Awali iliripotiwa kuwa wachezaji hao hawawezi kucheza mchezo huo, lakini sasa TFF inamaliza utata huo ambao ulishaanza kuwavuruga vijana wa Jangwani.
JAMII VIEWER
0 comments:
Post a Comment