Friday, 17 June 2016

Ray C aitia jamii simanzi na machozi

Leave a Comment


Msanii wa muziki Rehema Chalamila a.k.a Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya  kuzidisha madawa ya kulevya na kuanza kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa huku akitishia kuvua nguo.

Habari zinadai kuwa mama yake mzazi amekuwa akikesha kumtafuta mrembo huyo kutokana na kuzama kwenye vijiwe vya mateja wa madawa hayo na kushindwa kuonekana nyumbani.

Sambamba na hilo siku za hivi karibuni mwanamuziki Jay Dee, alionekana kuwa naye karibu na kudai kuwa Ray C, anahitaji marafiki wazuri na watu wavumilivu kuweza kumsaidia kwani kumlaumu pekee hakuwezi kumjenga bali ni kuzidi kumharibu kisaikolojia.

Mmoja wa wasanii wa Bongo Movie, Esha Buheti, kupitia mtandao wa kijamii ameweza kueleza jinsi gani alivyoguswa baada ya kumuoa Ray C akiwa chini ya ulinzi wa polisi akiwa hajitambui na kuongea maneno yasiyoeleweka na kudai kuwa awali alijua mrembo huyo anasingiziwa tuu.

Ameandika Nashindwa hata niongee nini jamani, Ray C leo Kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie Ray C, I mean it jamani siku zote nlikuwa najua anaonewa ila nilichokishuhudia leo nimeumia kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje?”

Akaendelea “Nilikua na Kabula, Kinondono kwa wapemba tumefuata chips mara tukasikia mtu anasema me Ray C nataka kuvua nguo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikuwa na nguvu sana watu kumshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafuta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaanza kugaragara kwenye matope akipiga kelele,”

“Kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari ya polisi ikambeba ila kwa tabu sana alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpaka Ray C anaondoka na ile gari ya polisi sikujua anapelekwa wapi alikuwa kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?”. 

Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:
"Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu? 

"We need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse @babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke me natamani aende rehab mwaka mzima) 

"Leo rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui amepelekwa wapi maskini 😢😢 atakua amelala wapi? Vipi kuhusu kesho Yake? Mamaake anajiskiaje? 

"Inaumaa jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa 🙏🙏🙏 tusaidiane  @rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari kujitolea kwa hali na mali my love"
                                                                              JAMII VIEWER
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: