Tuesday, 14 June 2016

rasmi mnyate kuchezea simba

Leave a Comment


NA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Jamal Simba Mnyate amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba sc Msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara ingawa ameweka wazi kuwa kuchelewa huko ni kwasababu kuna mambo walishindwa kufikia muafaka.

"Siku chache zilizopita nilikuja Dar kusaini, lakini tulishindwa kukubaliana na nikarudi Nyumbani Morogoro, nimekuja Dar jana nimesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuelewana. Kwahiyo kila kitu tayari na nimerudi zangu Morogoro, ila kila kitu fresh kabisa na Simba",amesema Mnyate

Usajili wa mchezaji huyo umeonekana kuwavutia mashabiki wengi wakati tetesi zikitawala kwamba atatua Msimbazi, wengi wao wamesifia na kusema anaweza kusaidia kwenye kikosi cha Simba
Simba pia imemsajili mlinzi wa Mwadui, Emmanuel Simwanza, ingawa kamati ya Usajili ya klabu hiyo inasema mambo yao ni kimya kimya.  JAMII VIEWER

If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: