Tuesday, 14 June 2016

Maguli simba- yanga njooni munisajili

Leave a Comment

NAMWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United, Elias Maguli, amesema yupo tayari kucheza katika klabu za Simba na Yanga, endapo zitaonyesha nia ya kumhitaji katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tayari klabu ya Mwadui FC imeonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo kwa msimu ujao ambaye tayari amemaliza mkataba na timu yake ya zamani Stand.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Maguli alisema kwa sasa yeye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na endapo ataafikiana na timu yoyote yupo tayari kwenda.
“Nilipigiwa simu na uongozi wa Mwadui FC ambao walifanya mazungumzo na mimi ya kuhitaji kwenda kucheza kwenye timu yao, lakini bado sijafanya maamuzi sahihi ya kukubaliana nao,” alisema.

Alisema endapo wataelewana atakuwa tayari kucheza kwenye kikosi hicho katika msimu ujao, kwani mpira ni ajira yake.
Maguli aliongeza kuwa kipindi hiki cha usajili kila timu ipo kwenye harakati za kusaka wachezaji, hivyo itakapotokea amekubaliana na timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu, watamalizana na kwenda kufanya kazi.
                                                                                        JAMII VIEWER
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: