Jana Maalim Seif Sharif ambaye ni raisi wa Zanzibar alishiriki katika mkutano wa CSIS nchini Marekani Washington DC ambapo alipata fursa ya kuongea kile kilichojitokeza katika uchaguzi wa tarehe 25 October 2015.
Katika mkutano huo uliojumuisha washiriki mashuhuri Duniani Maalim alieleza kwa kina namna ya democracy ilivyoekwa pembeni na watawala na kile walichoamua kukifanya na kukiita uchaguzi wa marejeo.
Maalim pia alieleza namna ya serikali ya Magufuli inavyoendeshwa ki detector na kutoa mfano wa kijana aliekamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwasababu tu ya kuongea ukweli katika account yake ya Facebook.
Pia akaendelea kusema kua viongozi wa chadema wamekua wakishtumiwa na kukamatwa na polisi kila mara na kusema kua hata yeye pia aliitwa kwa mahojiano ya masaa matutu na maafisa 11 wa polisi.
Baada ya kuzungumzia hali halisi inayoendelea Tanzania Maalim aliulizwa maswali mbali mbali na washiriki ambapo moja ya swali aliloulizwa ni lile wanalodai CCM kuogopa kumpa nchi kwasababu atavunja Muungano.
Maalim alieleza kua chama chake hakina lengo hilo bali lengo lake ni ku reform Muungano huu uliopo sasa na kwenda katika Muungano wa serikali tatu kama katiba ya Warioba ilivopendekeza.
Maalim alisema kua dhamira na lengo la Mwalim J.k. Nyerere lilikua ni serikali mbili kwenda moja lakini sera ya chama cha wananchi CUF ni serikali tatu kama katiba ya Warioba ilivopendekeza ingawa CCM wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu kuikubali katiba ile na kuamua kuzikataa dakika za mwisho jitihada na kazi mzuri iliofanywa na Warioba na kupewa baraka katika kila hatua na raisi Kikwete.
Maalim aliongeza kwa kusema kua hizo ni propaganda za CCM baada ya kuona kua kila njama na hila wanazozifanya ili kukiua chama cha wananchi CUF zinafeli na chama kinazidi kua imara zaidi na kusema kua CCM wanatumia ule msemo usemao kua "Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya" Yaani "If you want to kill a dog give him bad name".
Maalim alisema CCM awali walikua wakisema chama cha wananchi CUF ni chama cha kiislamu huku akibainisha kua pamoja na kusema hivo siku moja Ali Hassan Mwinyi aliwambia wakaazi wa Tanga kua CUF ni chama cha kitaifa na sio chama cha kiislam kwa kuamini kua kama angesema CUF ni chama cha kiislam angekua anakipigia kampeni chama hicho kwani waislam Tanga ni wengi.
Alipoulizwa kuhusu siasa kali na itikadi za kiislam na vitendo vya kigaidi vinavyoendelea duniani na mtazamo wake kuhusu hali ya Zanzibar ilivo sasa. Maalim alisema kua Zanzibar imepakana na nchi kama Kenya, Somalia na nchi nyengine amabazo vitendo vya kigaidi vimeshika kasi na kueleza hofu yake kua endapo vijana watahisi democracy haiwezi kuleta mabadiliko inaweza kua rahisi sana kwa vijana hao kushawishika kuingia katika vitendo hivo na kuzitaka Jumuia za kimataifa kuhakikisha kua democracy inafanya kazi Zanzibar.
Hata hivyo Maalim alisema kua pamoja na Wazanzibari kua asilimia 98 ni Waislam ila wamekua wakishirikiana kwa karibu sana na watu wa dini zote kama vile Hindu, Crustians na dini nyengine na kusema kua wanashirikiana pia hata katika shughuli mbali mbali za kijamii kama vile sherehe za harusi, mazishi nk.
Katika kufafanua zaidi swali hili Maalim alisema kua wailslam wa Zanzibar ni wastaarabu tofauti na nchi nyengine kwani mashehe wengi wa Zanzibar wamesoma ndani ya Zanzibar.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na raisi Magufuli na kile alichodai kua hawezi kuingilia mambo ya Zanzibar, Maalim alisema kua kwanza hakubaliani na maneno ya Magufuli ya kua haawezi kuingilia mambo ya Zanzibar na kusema kua Wazanzibari wanajiuliza kama kweli hawezi kuingilia mambo ya Zanzibar kapata wapi mamlaka ya kuleta jeshi wakati wa uchaguzi wa marejeo? Jeshi amabalo Maalim anasema idadi yake ilikua kubwa zaidi ya idadi ya Wazanzibari.
Pia aliendelea kusema kua kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio aliwahi kuomba kukutana na rais Magufuli na walikutana mara moja na mazungumzo yao yalikua ya kirafiki sana huku akimpa ushahidi wote wa ushindi wake na baadae rais Magufuli alimwambia Maalim endapo atahitaji kuongea nae tena atamwita. Katika hali hiyo Maalim anasema aliwahi kumuandikia tena barua sita raisi Magufuli akiomba kuonana nae lakini raisi Magufuli hakujibu hata barua moja.
Awali Maalim alitakiwa kuzungumzia mahusiano yake na Chadema (UKAWA)ambapo Maalim alisema kua uhusiano wao huo ulianza katika bunge la katiba ambapo mchakato wake ulisusiwa na vyama vinavyounda UKAWA baada ya chama tawala CCM kuyapinga maamuzi ya tume ya Jaji Warioba ambayo yalikubaliwa na kila upande wa Muungano bara na visiwani.
Baada ya hapo Maalim alieleza kua waliendelea kushirikiana na kuelekeza nguvu zao katika uchaguzi mkuu ambapo walisimamisha mgombea mmoja ambaye ni Mh. Edward Lowassa na kusema kua walifanya hivo kwasababu waliona kua wakisambaratika watakufa wote lakini wakiwa kitu kimoja wataweza kufanikiwa.
Akithibitisha hilo Maalim alisema kua UKAWA umeleta faida kubwa kwani chama cha wananchi CUF kimefanikiwa kupata wajumbe 10 wa bunge la Jamhuri ya Muungano ambapo awali walikua wakipata wajumbe wawili tu na kwa upande wa Chadema alisema kua idadi ya wajumbe wao wa bunge la Jamuhuri ya Muungano nayo pia imeongezeka.
Nae kwa upande wake balozi mstaafu wa Marekani nchini Tanzania Ambassador Green alisema kua aliwahi kuongea na rafiki yake mmoja ambae ni mkaazi wa Zanzibar kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 25 October na kumueleza kua hata wakishinda uchaguzi CUF, CCM haitokubali kutoa nchi na akaendelea kusema kua baadae baada ya kutokezea kile kilichotokea rafiki yake huyo alimpigia sim tena na kumuuliza je umeamini nilichokwambia? Balozi Green amesema baada ya kuona kile kilichotokea akaamini na kusema kua Zanzibar hakuna Mzanzibari yoyote alieamini kua CUF ingetendewa haki katika uchaguzi.
Hata hivyo kwa upande wake director wa CSIS Mh. Jennifer G. Cooke alisema bado raisi Magufuli anao wajibu na nafasi ya kuonyesha uongozi na kuingilia kati swala la Zanzibar ili liweze kutatuliwa. Alisema Marekani haina dhamira ya kuiadhibu Tanzania lakini pia haiko tayari kuiona Zanzibar inapata tabu (suffer).
Maalim Seif anatarajiwa kuendelea na ziara yake hiyo na kushiriki katika mikutano na maafisa na viongozi wengine wa serikali ya Marekani na Canada na kurudi baada ya siku 14 kama ratiba ya ziara hiyo inavyoelekeza.
Wazanzibari wengi wanaifatilia kwa karibu sana ziara hiyo huku wakiamini kua inaweza kuleta muelekeo na matumaini mapya ya Wazanzibari katika kuitafta na kuipata haki yao ya msingi ambayo imeporwa na CCM kupitia Jecha Salim Jecha.
Ni wajibu wa kila mtu kutoa mashirikiano na kuziunga mkono juhudi hizi za kiongozi wetu huyu mashuhuri anaependwa na kukubalika kila kona ya dunia.
Endapo kama tutatoka katika mstari na kuanza kupoteza umoja wetu katika kipindi hichi kigumu bila ya shaka tutakua tunazihujumu jitihada za kiongozi wetu huyu zenye maslahi mapana kwa nchi na taifa letu.
bofya ujionee
0 comments:
Post a Comment