Wednesday, 22 February 2017

Masogange aachiwa kwa Dhamana ya Milioni 10

Leave a Comment
Msanii  Agnes Gerald 'Masogange' amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka ya kutumia dawa za kulevya.

Mrembo huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 2i mwaka huu.
Katika mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan kwa nyakati tofauti.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yake, ameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Pia mrembo huyo ambaye amewahi kukamatwa nchini Afrika Kusini akihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya, ametakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam kwa kipindi chote cha kesi bila kibali cha mahakama.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: