Sunday, 5 June 2016

Yanga ya kimataifa yaongea watatu wa kimataifa

Leave a Comment
walter musona

NYOTA watatu kutoka Nigeria, Ghana na Zimbabwe wanatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili zijazo tayari kuanza mipango ya kujiunga na Yanga.

Mshambuliaji hatari Walter Musona raia wa Zimbabwe ambaye anakipiga katika kikosi cha FC Platinum amekubali kutua nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA msimu uliopita.
Lakini wachezaji wengine wawili, mmoja kutoka Ghana ambaye anaweza kutua nchini akiongozana na Kocha Hans van Der Pluijm keshokutwa Jumatatu. Huku yule wa Nigeria pia akitumiwa tiketi. Kikosini Yanga inao Wazimbabwe, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma.

Habari za uhakika zinasema Yanga iko tayari kuwaongeza hata wote ikiwezekana kama viwango vyao vitakuwa juu.
“Lakini nimeambiwa uongozi unataka kuwaleta wawili, hivyo kama ni chaguo basi itakuwa ni Musona pamoja na yule wa Ghana. Bado sijajua anatokea Madeama au Asante Kotoko,” alieleza mtoa habari.
Yanga inataka kujiimarisha katika safu ya ushambuliaji na kiungo na wawili hao ni viungo na mmoja ni mshambuliaji.
Uongozi wa Yanga umeendelea kuimarisha kikosi chake ili kuweza kupambana vilivyo katika michuano ya kimataifa baada ya kuingia katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kinachovutia zaidi, kamati ya ufundi ina uhakika wa kuona wachezaji hao wanasajiliwa baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusema yuko tayari kuachia fungu la kuimarisha kikosi chake.
Wakati huohuo taarifa kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa zimemuonyesha mlango wa kutokea kiungo mshambuliaji wake, Mniger Yossouf Boubacary kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa.
“Kweli hatujaridhika naye hata kidogo na tayari kocha amekubali aende zake. Sasa linabaki suala la uongozi kuamua utamalizana naye vipi,” kilieleza chanzo.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: