Thursday, 9 June 2016

Yanga imepanga kuwapiga bao simba kwa Telela

Leave a Comment


Salum Telela ameshindwa kuzungumzia ‘mustakabali’ wake baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga SC. Nahodha huyo wa zamani wa timu za Taifa za vijana na klabu ya Moro United ameshinda mataji mengi katika misimu yake 6 akiwa na timu hiyo iliyomsaini akiwa kinda mwaka 2010 akitokea Moro United.
Salum Telela anajua kwamba anafuatiliwa sana kwa karibu na club ya simba. na alimuambia mwandishi wetu>>>>>>>
“Nimecheza kwa misimu 6 katika timu hii na nimepata mafanikio makubwa ikiwemo ushindi wa mataji ya ligi kuu (2010/11, 2012/13, 2014/15, 2015/16,) nimeshinda Kagame Cup 2011 na 2012, Ngao ya Jamii 2013, 2014, 2015, pia taji moja la FA.”<<<<<<<<<
“Msimu uliopita kulikuwa na ushindani mkubwa sana lakini niliweza kupambana na kucheza zaidi ya michezo 20. Ukitazama hata uwiano wa mechi kwa wachezaji wa nafasi yangu hazikupishana sana. Nilikuwa na msimu mzuri. Pia nafurahi kufanya kazi na kocha mzuri kama Hans Van der Pluijm na kila mmoja katika benchi la ufundi.”Nilimuuliza, Telela, ni kweli unaondoka Yanga? lakini akajibu kwa namna ya kutohitaji kuzungumzia mambo ya usajili. “Habari hizo naomba tuachane nazo, ni mapema kujadili hayo.”
Telela amekuwa akiwindwa na Simba lakini Yanga wamepanga kukamilisha usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii.
Fanya kulike page hii ili upate updates ya sakata hili la Salum telela.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: