Simba ina mtazama Shomari kama mmoja wa wachezaji muhimu wajaye katika kikosi chao ambao watasajiliwa ili kuinyanyua tena timu hiyo iliyopoteza mwelekeo katika msimu minne mfululizo iliyopita.
‘Wekundu wa Msimbazi’ walizidiwa kete dakika za mwisho na mahasimu wao Yanga SC baada ya kuwasaini, golikipa Beno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya na mlinzi wa kati Vicent Andrew kutoka Mtibwa.
Ikiwa imehamishia nguvu zake katika timu za Prisons inakowasaka mshambulizi, Jeremiah Juma na kiungo wa pembeni Mohamed Mkopi, Simba inataka kuwasaini kwanza Shomari ili kuchukua nafasi ya beki namba 2 iliyoachwa na Hassan Kessy aliyetimkia Yanga, naKichuya kwa lengo la kuimarisha safu ya kiungo na ile ya mashambulizi.
“Ni kweli Simba inawahitaji Shomari na Kichuya lakini vijana wenyewe hawako tayari kuondoka hapa (Mtibwa,) chini ya milioni 30 si rahisi wachezaji hao kujiunga Simba. Kwanza wana wasiwasi kwa kutazama misukosuko iliyowakuta wachezaji wengine katika timu hiyo.” anasema mmoja kati ya marafiki wa karibu wa wachezaji hao.
Habari ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba, Mtibwa haitakuwa tayari kuwaachia wachezaji wake wenye mikataba huku wakipanga dau lisilopungua milioni 20 kwa kila mchezaji anayetakiwa na klabu kubwa.
Shomari ambaye alikuwa wing namba 7 wakati Kessy akicheza katika beki 2 pale Mtibwa, amekuwa na msimu mzuri akicheza kama namba mbili msimu huu na Simba imekuwa ikivutika naye.
Kichuya ni mchezaji ambaye alishinda tuzo moja kama mchezaji bora wa Mwezi katika ligi kuu Tanzania Bara iliyomalizika ni mchezaji ambaye anaweza kuinyanyua timu na kuipa matokeo mazuri.
0 comments:
Post a Comment