Kwa ubora uliowapatia Yanga ubingwa msimu uliopita, ni dhahiri kuna wachezaji ambao walikuwa chachu ya mafanikio ya klabu hiyo kufika ilipo
Wachezaji watano bora walifanya vizuri msimu 2015/16 kwenye kikosi cha Yanga, na Goalinapenda kukuletea uchambuzi wa wachezaji hao mahiri.
1. Deogratius Munish ‘Dida’
Huyu ni kipa chaguo la kwanza la kocha Hans van der Pluijm, msimu huu alikuwa kwenye kiwango bora na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika kwa kupangua penalty katika mchezo wa marudiano na timu ya Sagrada Esperanca ya Angola ambayo ilimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0 na mabingwa hao wa Tanzania kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Didia pia alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, ambao ulikuwa wa marudiano na wenyeji iliwabidi kusubiri hadi dakika za nyongeza ili kupata bao la ushindi na Yanga kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 na ndipo ilipoangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
2. Donald Ngoma
Kati ya wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwenye mafanikio ya Yanga msimu huu basi huwezi kuliacha jina la Ngoma ambaye ameonyesha uwezo mkubwa msimu huu ikiwemo kufunga bao pekee kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Yanga kufunga bao kwenye aridhi ya Misri.
Lakini mchango wa Mzimbabwe huyo umechangia kuiweka Juu Yanga ambapo kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ndiyo timu pepee inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi CAF.
3. Juma Abduli
Fulback wa kushoto ambaye huwezi kuzungumza mafanikio ya Yanga msimu huu bila kuuona mchango wake, mlinzi huyo wa kushoto amefanya kazi kubwa msimu huu kwa kuipigania timu hiyo na krosi zake ndizo zilizomwezesha Amissi Tambwe kuwa mfungaji bora msimu huu.
Juma pia ndiyo aliyewasumbua Al Ahly na krosi yake iliweza kutumiwa vyema na Donald Ngoma kuisawazishia Yanga bao ilipokuwa ugenini Alexandira ingawa walipoteza mchezo huo baada ya dakika 90.
4.Thabani Kamusoko
Mmoja ya nembo ya Yanga msimu huu na hiyo ni kutokana na uwezo wake aliokuwa nao wa kuichezesha timu na kutoa pasi za mwisho kwa wafungaji au mara nyingine kufunga yeye mwenye.
Ubora wa Kamusoko unaweza kuuona pale Yanga inaposhambulia au inapozidiwa kwani amekuwa na uwezo mkubwa wakubadilisha mpira na kuwachanganya wachezaji wa timu pinzani wasijue cha kufanya.
5.Amissi Tambwe
Mshambuliaji aliyejizoelea umaarufu Tanzania kutokana na uwezo wake aliokuwa nao wa kufunga mabao, kwa kiwango alichokionyesha Tambwe msimu huu anaingia katika wachezaji bora watani waliosaidia mafanikio ya Yanga msimu huu.
0 comments:
Post a Comment