Friday, 17 June 2016

Simba sc yapiga panga hawa wachezaji

Leave a Comment


Uongozi wa Simba umekubaliana wachezaji ambao walionekana ni tatizo ndani ya kikosi hicho, watatemwa ili kuanza upya.

Taarifa za uhakika zimesema, uamuzi wa kuchukua maamuzi magumu ili kuhakikisha wanaondoa figisu ndani ya kikosi chao.

“Kweli wamepitisha uamuzi huo, ingawa kuna wale walikuwa wakitaka wachezaji fulani wabaki lakini kuna wengine wamepinga kabisa.

“Unajua Simba wana uthibitisho wa mambo mengi sana katika mechi za mwisho ambazo wamefanyiwa. Lakini hawawezi kuweka hadharani kila wanachokijua.

“Ukweli ni kwamba kulikuwa na hujuma na wachezaji walitumika sana na kuna wale ambao walikuwa wanaonekana kuwa vinara wa kufanya hujuma. Sasa kuwabakiza ni kujimaliza,” kilieleza chanzo.

Kati ya watakaopitiwa na panga, imeelezwa ni wachezaji wa nyumbani na wa kigeni wakiwemo wale ambao walionekana ni tegemeo kubwa katika kikosi hicho.


Hofu ya uongozi wa Simba ni kuwabakiza wale ambao wanaonekana kuwa makini ili kuepuka kuwabakiza waliowaona kuwa ni tatizo kubwa kwao.
                                                                                                JAMII VIEWER
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: