Saturday, 11 June 2016

Niyonzima awa mwalimu wa kessy aliesaini yanga akitokea simba

Leave a Comment

Kiungo mchezeshaji wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amemwambia beki wa timu hiyo, Hassani Kessy kuwa asahau maisha ya Simba na badala yake akili na mawazo yake aelekeze kwenye klabu yake mpya anayoichezea hivi sasa.


Kauli hiyo, aliitoa jana kwenye mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakati timu ikijifua na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia utakaopigwa Juni 17, mwaka huu huko Algeria.

Kessy alisaini kuichezea Yanga wiki tatu zilizopita akitokea Simba.
Niyonzima alisema, Kessy ni bonge la mchezaji, lakini kikubwa anachotakiwa ni kuzoea mazingira haraka ya timu, pia aendane na kasi ya Yanga ili apate nafasi ya kucheza.

Niyonzima alisema, pia beki huyo anatakiwa kupambana ndani ya uwanja pale atakapopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ili amshawishi kocha kumuamini zaidi.

“Nikwambie kitu, Kessy ni bonge la mchezaji na ni kati ya mabeki ninaowakubali kabla ya kusaini kuichezea Yanga, kikubwa anachotakiwa ni kupambana ndani ya uwanja ili apate nafasi ya kucheza.

Pia aliongeza kuwa kwasababu yeye bado ni mdogo hiki ndicho kipindi chake muafaka cha kutengeneza maisha yake kwa kutumia soka, hivyo anatakiwa kuongeza mazoezi ili atengeneze soko lake.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: