Friday, 10 June 2016

Mnyate asaini msimbaizi

Leave a Comment

Klabu ya Simba, imefanikiwa kuinasa saini ya winga mwenye kasi wa Mwadui FC, Jamali Mnyate aliyesaini mkataba wa miaka miwili kwa ada ya Tsh. Milioni 15.
Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema, tayari wamemaliza zana na mchezaji huyo na sasa ni mali yao.
“Baada ya kuondoka Ramadhani Singano tulimkosa mtu mwenye kasi na msimu uliopita tumepata sana tabu ndiyo maana tukakubaliana kumsajili Mnyate ambaye kwa kiwango alichonacho tunaamini atatusaidia katika mipango yetu ya kurudi kwenye ubora wetu msimu ujao,”amesema Kaburu.
Kaburu amesema walikuwa wakimfukuzia kwa muda mrefu mchezaji huyo na wanafurahi kuona wameipata saini hiyo ikiwa ni muda muafaka baada ya timu yao kuwa na mapungufu mengi ambayo kwasasa ndiyo wanayafanyia kazi kipindi hiki cha usajili.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: