Atupele amesema kwamba anashangazwa na uvumi kwamba yeye hawezi kuchezea Simba kwa madai eti ana mapenzi na Yanga.
“Ninashangazwa sana na huu umbeya. Mimi ni mchezaji na soka ndiyo ajira yangu, niko tayari kusaini timu yoyote, nachoangalia ni maslahi,”amesema“Mimi Yanga nilipita nikiwa mdogo na sikukaa sana, nilipoona umri wangu sasa umefikia kucheza Ligi na pale siwezi kupata nafasi, nikaenda timu nyingine nimecheza nimekuza uwezo wangu na kupata uzoefu wa kutosha na sasa watu wanamjua Atuepel ni nani,”.
Atupele amesema Simba kama wanamtaka wamfuate kwa mazungumzo na kama wakiafikiana basi watamhukumu kwa shughuli yake uwanjani.
“Mimi kama mchezaji kazi yangu inaonekana uwanjani, waje tuzungumze, tukikubaliana tuingie Mkataba halafu waone kazi yangu siku tukikutana na hao Yanga,”amesema mchezaji huyo aliyemaliza Mkataba wake Ndanda FC ya Mtwara.
Atupele aliyewahi kuchezea Yanga B baada ya kusajiliwa kwa dau la rekodi kwa wachezaji vijana, Sh. Milioni 17, amecheza Ndanda FC kwa msimu mmoja tu akitokea Kagera Sugar
0 comments:
Post a Comment