Tuesday, 7 June 2016

kwa mawindo haya mnyama lazima aungurume 2016-2017

Leave a Comment
Wachezaji wa Azam wakiwa wamembeba shujaa wao wa leo Malika Ndeule baada yakutoka kifua mbele zidi ya simba

NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Simba umemalizana na beki wa Mwadui, Malika Ndeule na sasa imeelekeza nguvu zake kwa beki Rashid Mandawa wa Kagera Sugar na Jeremia Juma wa Prisons. Mbali na wachezaji hao pia Simba ipo kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji Ibrahimu Jeba na Chiza Kichuya wote wa Mtibwa Sukari.
Habari za kuaminika ambazo HabariLeo imezipata zinasema kuwa, Simba imepanga kuibomoa Mtibwa kwa kuchukua wachezaji wake watano, huku kwa Prisons ikisaka saini ya Jeremia ambayo pia inasakwa na Azam FC.
Jeremia ni kati ya wachezaji waliong’ara katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliomalizika, akifunga mabao 11 nyuma ya Kipre Tchetche wa Azam raia wa Ivory Coast. Mrundi Amissi Tambwe wa Yanga ndiye ameibuka kinara wa upachikaji mabao baada ya kufunga mara 21, akifuatiwa na Mganda Hamisi Kiiza aliyefunga mabao 19, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma na mzalendo Elias Maguri waliofunga mabao 14 kila mmoja
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: