Klabu hizo ni Al Ahly na Zamalek ambazo kwa sasa zipo katika vita kubwa ya kuwania saini ya mshambuliaji huyo aliyengara msimu huu akiwa na Yanga aliyoipa mafanikio makubwa ikiwemo kuipeleka hataua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga, ameiambia Goal hadi sasa hawajapokea maombi kutoka klabu yoyote kati ya hizo mbili kumtaka mchezaji huyo na endapo yatafika watayafanyia kazi na kuyatolea majibu kama watamuuza au vinginevyo.
“Tunasikia taarifa hizo kupitia kwenye mitandao mbalimbali na vyombo vya habari lakini rasmi hatujapokea barua kutoka klabu yoyote inayomzungumzia Ngoma ikitokea tutakaa kama uongozi na benchi la ufundi kujali kama tumuuze au vinginevyo,”amesema Sanga.
Ngoma amebakiza msimu mmoja wa kuitumikia Yanga, inadaiwa tayari ameanza mazungumzo ya awali na klabu ya Al Ahly iliyovutiwa zaidi na uwezo wake lakini Zamalek nao wameingilia kati mbio hizo na wao wameanza mipango ya kuja Tanzania kukutana na uongozi wa Yanga ili kumnasa mchezaji huyo aliyefunga mabao 21 katika mashindano yote msimu huu.
0 comments:
Post a Comment