Saturday, 18 June 2016

kiungo mpya ataka kuwasotesha benchi Mkude na Ndemla

Leave a Comment


IUNGO mpya wa Simba, Mzamiru Yasini, amesema, hayupo tayari kukaa benchi na atahakikisha anapambana na wakongwe ili kucheza kikosi cha kwanza.
Mzamiru ametua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar, na changamoto kubwa inayomkabili ni kuwania namba na Jonas Mkunde, Justice Majbvi na Said Ndemla.
Alisema, kiungo huyo aliyeng’ara na Mtibwa msimu uliopita, alisema anafahamu changamoto anayoenda kukutana nayo kwenye timu hiyo na tayari ameanza kujipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili kumshawishi kocha aweze kumpanga kikosi cha kwanza.
“Naenda Simba nikifahamu nafasi yangu ina wachezaji wengi wazuri na wana uzoefu, lakini nimejipanga kumshawishi kocha aweze kunitumia kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu nisingependa kukaa benchi ,”alisema Mzamiru.
Kiungo huyo alisema anafahamu Simba ni timu kubwa, ambayo mashabiki wake wanahitaji ushindi kila siku, hivyo atajitahidi kwa kushirikiana na wenzake wanapigana na kurudisha mataji ambayo yamekuwa adimu kwa misimu mitatu iliyopita.
Aliwaomba mashabiki wa timu hiyo kumpa sapoti ili aweze kutumia vizuri kipaji alichokuwa nacho kwa ajili ya kuwapa raha na kusahau machungu waliyoyapata siku za nyuma.
Huyo ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao, wachezaji wengine wawili ambao tayari wameshatua Msimbazi ni Emmanuel Semwanza na Jamal Mnyate kutoka Mwadui FC ya Shinyanga.
                                                                                           JAMII VIEWER
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: