Wednesday, 1 June 2016

Donald Ngoma wa Yanga akaribia kutua Al Ahly ya Misri

Leave a Comment




Habari kutoka Misri zinaashiria kwamba Al Ahly wanaitamani saini ya mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma
Mshambuliaji wa Zimbabwe amekuwa kivutio kikubwa akiwa na klabu bora ya Tanzania Yanga tangu alipotua Jangwani akitokea FC Platinum. Amefunga mabao 17 katika msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom 2016/16, matatu katika Ligi ya Mabingwa ikiwa ni pamoja na goli safi la kichwa dhidi ya Al Ahly na moja Kombe la FA.
Katika mahojiano na Marwan Ahmed wa Kingfut.com Ngoma amesema yupo tayari kwenda Misri.
“Kwa nini hapana? Ni klabu kubwa katika Afrika na nitakuwa tayari kwenda Misri,” alisema Ngoma.
Mabingwa wa sasa wa Misri Al Ahly wataingia sokoni mwisho wa msimu huu, kumsaka mshambuliaji huyo wa kimataifa baada ya washambuliaji wao wa kigeni Malick Evouna kutoka Gabon na John Antwi kutoka Ghana kushindwa kuonyesha umahiri wao.
If You Enjoyed This, Take 5 Seconds To Share It

0 comments: